Arsenal wanunua kiungo wa FC Basel

Elneny Haki miliki ya picha Getty
Image caption Elneny anaweza kuchezea Arsenal dhidi ya Stoke Jumapili

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.

Mchezaji huyo anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.

Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anahitimu kuwachezea katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Akizungumza baada ya Arsenal kutoka sare ya 3-3 na Liverpool uwanjani Anfield, Wenger alisema: "Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anatosha kucheza Jumapili.”

Haki miliki ya picha Reuters

Elneny alichezea Basel mechi ambayo walilaza Chelsea msimu wa 2013-14.