Wada: Wakuu wa IAAF walijua kuhusu dawa

Dick Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkuu wa Wada Dick Pound amesema ufisadi IAAF ulianza kwa rais wa shirikisho hilo

Shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa katika riadha duniani imesema wakuu wa shirikisho la riadha duniani IAAF walifahamu kuhusu uozo katika shirikisho hilo.

Shirika hilo, WADA, linasema mkuu wa zamani wa IAAF Bw Lamine Diack, "alipanga na kuwezesha mpango wa kuhujumu haki na pia kufanikisha ufisadi” katika shirikisho hilo.

Bw Diack, ambaye ni raia wa Senegal alikamatwa na kushtakiwa nchini Ufaransa mwezi Novemba.

Haiwezekani baraza kuu la IAAF liwe halikufahamu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini katika riadha pamoja na kutotekelezwa kwa sheria za kuzuia matumizi ya dawa hizo"

Ripoti ya Wada kuhusu ufisadi katika IAAF
AP

Ripoti ya Wada imesema baraza kuu la "lazima lilikuwa na ufahamu” kuhusu kuenea kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli.

Rais wa sasa wa shirikisho hilo, Sebastian Coe, alikuwa kwenye baraza hilo, na alihudumu kama makamu wa rais chini ya Lamine Diack.