Je,Crystal Palace itamnunua Adebayor?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Adebayor

Mkufunzi wa kilabu ya Crystal Palace amesema katika mkutano na vyombo vya habari kwamba hapingi mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Togo Emmanuel Adebayor kutoka Tottenham Hotspur.

Adebayor hajacheza msimu huu baada ya Tottenham kusema kwamba hayuko katika mipango yao.

''Yupo huru kwa yeyote yule kumuona,swali ni je? Je, kilabu yetu itamfaa ,na je, ni mchezaji tunayemsaka? Hatuwezi kumpinga yeyote,alisema Allan Pardew.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alan Pardew

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya aliyekuwa kocha wa Adebayor Harry Rednapp kusema kuwa atakayemsajili mchezaji huyo 'hatumii akili'.