Andy Carroll kukaa nje wiki sita

Carroll Haki miliki ya picha Getty
Image caption Carroll amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha

Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll huenda akakaa nje kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia misuli ya paja.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliondolewa uwanjani baada ya kucheza dakika 15 pekee mechi dhidi ya Bournemouth, ambayo walishinda 3-1.

Carroll, 27, alikuwa amewafungia West Ham mabao mawili katika mechi zake nne za majuzi zaidi baada ya kurudi kucheza Septemba 2015.

Kabla ya hapo, alikuwa amekaa miezi saba nje baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake.

“Mambo yakienda tunavyotarajia, basi atatusaidia mechi 10-15 za mwisho msimu huu,” amesema meneja wa West Ham Slaven Bilic.

Haki miliki ya picha Getty

Carroll, ambaye aliwahi kuchezea Newcastle, Carroll alijiunga na West Ham kutoka Liverpool kwa £15m mwezi Juni 2013.

West Ham wamo nambari tano ligini, alama moja pekee nyuma ya Tottenham walio nambari nne, zikiwa zimesalia mechi 17 za kuchezwa msimu huu.