Larsson amtupa nje Watson

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Heather Watson

Ndoto za mwingereza Heather Watson, kutetea taji la michuano ya kimataifa ya tenisi Hobart, zimefutika baada ya kuchapwa na Johanna Larsson wa Sweden.

Larsson anayeshika nafasi ya 54 kwa ubora alipata ushindi huo licha ya kupoteza seti ya kwanza kwa 3-6 kisha akashinda kw 6-4 na 6-4. Hii ilikua ni mechi ya pili kwa Watson anayeshika nafasi ya 53 kwa ubora wa viwango baada ya kumshinda Monica Niculescu, katika mchezo uliopita. Mchezo huo wa robo fainali ulitumia muda wa saa tatu na dakika kumi na tatu.