Madrid ya Zidane yaiua Sporting Gijon

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kocha wa Real Madrid, Zinedin Zidane

Klabu ya soka ya Real Madrid imefanikiwa kuizamisha Sporting Gijon katika mwendelezo wa ligi kuu ya Hispania kufuatia ushindi mnono wa mabao 5-1 ambayo yamefungwa na wachezaji Gareth Bale bao 1 , chirstiano Ronaldo mabao 2 pamoja na Karem Benzema akifunga mabao 2.

Na klabu ya Barcelona imekwea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kufuatia ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Althltic Bilbao,mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Lionel Messi , Neymar da Silva Santos , Luis Alberto Suárez , na Ivan Rakitic .