Liverpool kuchuana na Man United

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liverpool dhidi ya Man United

Beki wa Liverpool Dejan Lovren anakaribia kurudi baada ya jeraha lakini hatashiriki katika mechi dhidi ya Manchester United siku ya jumapili.

Hakuna mchezaji ambaye amekuwa akiuguza jereha ambaye atashiriki katika mechi hiyo kwa upande wa Liverpool huku Daniel Sturridge akiendelea kuuguza jereha.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liverpool ikikabiliana na Manchester United

Manchester United nayo itajibwaga uwanjani bila kiungo wa kati Bastian Schweinsteiger ambaye anauguza jereha la goti,huku kiungo wa kati mwengine Michael Carrick akiwa amejeruhiwa.

Beki Phil Jones anatarajiwa kurudi baada ya kupata jereha la mguu.