Udanganyifu kwenye tenisi wabainika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ushahidi umetolewa kubainisha uwepo wa udanganyifu kwenye mchezo wa Tenis

Uchunguzi uliofanywa na BBC na mtandao wa Buzz Feed ,umebainisha kuwepo kwa ushahidi wa udanganyifu na kupanga matokeo ya mechi katika mashindano ya tenisi duniani ikiwemo shindano la Wimbledon.

Nyaraka za siri zimeonyesha kuwa katika muongo mmoja uliopita wachezaji kumi na sita wametambuliwa na maafisa wanaosimamia mchezo huo kwa hofu ya kukubali kushindwa kwa hiari.

Lakini Idara ya kupambana na ufisadi ya mchezo huo imesema imekuwa ikichukua hatua kali dhidi ya dalili zozote za kupanga matokeo na ufisadi unaohusiana na mchezo wa kamari.

Hii inatokana na matokeo ya uchunguzi yaliyoanzisha mwaka 2007 na Chama cha Wataalamu tenisi cha (ATP).