Leicester kumsajili beki wa Ghana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Daniel Amartey

Beki wa timu ya taifa ya Ghana Daniel Amartey anakaribia kujiunga na kilabu ya ligi kuu ya Uingereza Leicester City.

Kilabu ya Amarte Denmark FC Copenhagen ,imekubali kumuuza kwa Leicester ambayo ipo katika kilele cha ligi ya Uingereza.

''Ni miongoni mwa mipango yetu kama kilabu kuwakuza wachezaji hadi kiwango ambacho kinavutia timu nyengine kutoka katika ligi kubwa ambazo huwanunua kwa kitita kikubwa cha fedha'',alisema Meneja mkuu wa kilabu hiyo Anders Horshlt katika taarifa.

Amartey ambaye ameichezea FC Copenhagen mechi 63,anatarajiwa kuweka makubaliano ya kibinafsi na Leicester kabla ya mkataba wake kuidhinishwa.