Tunisia yatoka sare na Guinea

Image caption Chan2016 mchezaji wa tunisia

Guinea ilifunga katika muda wa lala salama na kupata droo ya 2-2 dhidi ya Tunisia katika mechi ya kundi Cha katika mashindano ya soka barani Afrika miongoni mwa wachezaji wanaosakata soka barani.

Ahmed Akaichi wa Tunisia alifunga bao la kwanza katika dakika ya 32 mda mfupi baada ya kombora lake kupiga mlingoti wa goli.

Hatahivyo Alseny Kamara aligusa pasi nzuri na kusawazisha kunako dakika 39,lakini baada ya muda wa mapumziko Akaichi aliimarisha azma ya Tunisia alipofunga bao la pili.

Guinea ilinusurika baada ya kichwa cha Zied Boughatt kupiga mlinghoti wa goli kabla ya Tunisia kupata bao la kusawazisha wakati Camara alipofunga bao la pili kutoka kwa kona.

Huku pointi hiyo ikishabikiwa na Guinea,mashabiki watakuwa na wasiwasi baada ya Camara kubebwa na kutolewa nje ikiwa imesalia dakika 3 na watatumai kwamba yuko vyema ili kuweza kuendelea na mechi hizo.