Tambwe kinara wa mabao Yanga

Image caption Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Tambwe

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Mrundi Hamisi Joselyn Tambwe ameendelea kuwa kinara wa kupachika mabao katika klabu yake ya wanajangwani Yanga SC.

Tambwe amefanikiwa kuirejesha timu hiyo kileleni mwa Ligi kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Timu ya Majimaji katika mchezo uliopigwa jana uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, yeye akipachika mabao 3 katika ushindi huo.

Kwa ushindi huo Yanga imerudi tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kufikisha alama 39, sawa na Azam FC iliyopo nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao.

Hamisi Tambwe amesema kuwa bado ataendelea kufunga magoli mengi ili kuipatia timu yake ushindi katika kila timu atakayokutana nayo, amesema kuwa kama mchezaji juhudi zake zote ameziweka uwanjani na kuheshimu kama kazi yake hivyo hana budi kutafuta nafasi za kufunga pamoja na kuwatafutia washambuliaji wengine nafasi za kufunga pia na kuhakikisha timu yake inatwaa ubingwa