CHAN2016:Uganda yalazwa,Mali yashinda

Image caption Mashabiki wa Uganda baada ya timu yao kulazwa

Mali imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika kundi la 4 mechi iliyochezwa mjini Rubavu.

Goli hilo lilipatikana kunako dakika ya 82 na kufungwa na mshambuliaji Moussa Sissoko.

Kwa ushindi huo Mali sasa inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 4 kabla ya pambano kati ya Uganda yenye alama 1 na Zambia yenye alama 3.

Wakati huohuo Zambia imekata tiketi yake ya robo fainali kwa kuishinda Uganda 1-0 mjini Rubavu.

Goli hilo limefungwa na mkongwe Christopher Katongo kunako dakika ya 41 ya mchezo.

Image caption Michuano ya Chan Rwanda

Bahati ya Uganda kuvuka ngazi ya mchujo ni finyu sana.

Uganda italazimika kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Zimbabwe na kutegemea Zambia kuishinda Mali ilhali Mali itahitaji tu matokeo ya sare.