Leicester yamsajili beki wa Ghana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Daniel Amartey

Kilabu ya Leicester City hatimaye imemsajili beki wa taifa la Ghana Daniel Amartey kutoka kilabu ya FC Copenhagen nchini Denmark kwa kitita kisichojulikana.

Amartey anaweza kucheza katikati na anaaminika kuigharimu kilabu hiyo pauni milioni 6.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye ameichezea timu yake ya taifa mara 6 aliichezea FC Copenhagen mechi 63 baada ya kujiunga na kilabu hiyo mwaka 2014.

''Daniel amekuwa kiungo muhimu katika timu yetu'',alisema Meneja wa Copenhagen Stale Solbakken.

Image caption Mashabiki wa Leicester

''Ni ndoto yake kwa yeye kucheza katika ligi ya Uingereza na katika kilabu ambayo imekuwa ikimsaka kwa muda mrefu''.

Amartey ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Leicester katika dirisha la uhimisho la mwezi Januari baada ya winga Damarai.