Mchezaji mwenye chongo ashiriki mechi Uturuki

Image caption Emre Azim

Ushindi wa Fenerbahce wa taji la ligi ya Uturuki huenda sio muhimu sana ,lakini kile kitakachokumbukwa na wengi kuhusu mechi hiyo ni kucheza kwa mara ya kwanza kwa mchezaji mwenye chongo.

Emre Azim wa kilabu ya Tuzlaspor mwenye umri wa miaka 18 alishiriki katika mechi dhidi ya Fenerbahce katika dakika chache za mwisho.

Fenerbahce ilishinda mechi hiyo 1-0 huku mchezaji wa liverpool ambaye anaichezea kilabu hiyo kwa mkopo Lazar Markovic akifunga bao hilo.

Kikiwa kisa cha kipekee,haijawahi kutokea kwa mchezaji mwenye chongo kushiriki katika ligi ya kulipwa.

Mshambuliaji wa Ireland Kaskazini Dean Shiels alifanyiwa upasuaji kuondoa jicho lake la kulia mwaka 2006,baada ya kujeruhiwa alipokuwa na miaka minane.