Chelsea yaichapa Arsenal

Haki miliki ya picha AP

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chelsea walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal wakiwa ugenini.

Arsenal walicheza mchezo huu wakiwa pungufu baada ya mlinzi wao Per Mertesacker, kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.

Upungufu huo ulimfanya kocha Arsene Wenger, amtoe mshambuliaji Olivier Giroud, na kumwingiza mlinzi Gabriel Paulista.

Arsenal wameshindwa kufuta uteja kwa chelsea na kumewapeleka timu hiyo kushika nafasi ya tatu wakiwa na alama 44 huku Man City, wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 44 na vinara ni Leicester City wakiwa na alama 47 kibindoni.