Ramires kujiunga na Jiangsu Suning

Image caption Ramires Santos do Nascimento

Kiungo wa kimataifa wa Brazil na klabu ya soka Chelsea Ramires Santos do Nascimento anakaribia kujiunga na timu ya Jiangsu Suning ya China.

Kiungo huyu mwenye miaka 28 alisajiliwa na Chelsea toka Benfica, mwaka 2010 kwa pauni la pauni milion 17 na inatarajiwa timu hiyo inayocheza ligi kuu ya china iko tayari kutoa dau la pauni million 25 kumnasa nyota huyo.

Ramires, alisaini mkataba mpya wa miaka minne mwezi Octoba,mwaka jana, ila ameanza kikosi cha kwanza kwenye michezo saba tu msimu huu wa ligi ya England.

Timu ya Jiangsu ilimaliza katika nafasi ya nane kwenye msimu wa mwaka 2015, na kikosi hicho kinanolewa na nyota wa zamani wa Chelsea Dan Petrescu.

Kiungo huyu wa kibrazil akiwa na The Blues, ametwaa ubingwa wa ligi, kombe la Fa,kombe la ligi , ubingwa wa klabu bingwa ulaya na ile michuano ya Europa ligi.