Rooney na mkewe wajaliwa mtoto mvulana

Rooney Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rooney alifungia Man Utd bao dhidi ya Liverpool tarehe 17 Januari

Mke wa nahodha wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Wayne Rooney amejifungua mtoto mvulana.

Mtoto huyo amepewa jina Kit Joseph Rooney.

Mwanasoka huyo alitangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo Jumapili usiku kupitia mtandao wa Twitter, ambako anafuatwa na watu 12.5 milioni.

Haki miliki ya picha PA

Rooney mkewe Coleen tayari wana watoto wawili wa kiume, Kai mwenye umri wa miaka sita na Klay mwenye umri wa miaka miwili.

Mapema Jumatatu, alipakia picha ya mtoto huyo kwenye Twitter, baada yake kumuona mara ya kwanza, na kuandika: “Kukutana na Kit kwa mara ya kwanza. Twaenda nyumbani sasa”.