Wenger: Costa alitutonesha kidonda tena

Image caption Wenger: Costa alitutonesha kidonda tena

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amelalamika vikali dhidi ya hujuma na ushari wa mshambulizi machachari wa Chelsea Diego Costa aliyesababisha mchezaji wake Per Mertesacker kutimuliwa mapema katika mechi hiyo iliyochezwa ugani Emirates.

Chelsea ilibuka washindi wa bao moja kwa nunge.

Mfungaji wa bao hilo alikuwa ni mshambulizi huyo mbishi Diego Costa.

Mertesacker aliamrishwa kuingia bafuni mapema baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza kwa kumuangusha Costa.

''Mwenye macho haambiwi tazama alifoka Wenger.

''Costa amesababisha wachezaji wetu 2 kutimuliwa katika mechi mbili dhidi ya Chelsea,'' Alisefoka Wenger.

''Je ilikuwa haki ?

'Sijui.'

'Ila ninachokifahamu ni kuwa Gabriel alitimuliwa katika kichapo cha 2-0 dhidi yao mnamo mwezi wa Septemba.'

Haki miliki ya picha PA
Image caption ''Costa amesababisha wachezaji wetu 2 kutimuliwa katika mechi mbili dhidi ya Chelsea,'' Alisefoka Wenger.

''Simtuhumu kwa kufanya kosa lolote.''

Kufuatia kuondoka kwa Mertesacker mapema sana katika mechi hiyo, Arsenal ilipoteza kasi mbali na uongozi wake kileleni mwa ligi kuu.

Arsenal sasa wameshuka hadi nafasi ya 3 wakiwa na jumla ya alama 44.

Manchester City ambao walisajili ushindi muhimu wamewapiku Arsenal kutoka nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.

Arsenal sasa wanashikilia nafasi ya 3 nyuma ya Leicester na Man City.

Kadi hiyo nyekundu dhidi ya Mertesacker ni ya saba dhidi ya mchezaji wa Arsenal.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption ''Kwa hakika refarii alikuwa mwepesi sana kutuadhibu ila ninafikiri ilikuwa chanzo cha kushindwa kwetu'' alisema Wenger.

''Kwa hakika refarii alikuwa mwepesi sana kutuadhibu ila ninafikiri ilikuwa chanzo cha kushindwa kwetu'' alisema Wenger.

Sina hakika iwapo Costa alikuwa keshaotea ama iwapo Per Mertesacker alimgusa au la,Wakati mwengine mkifungwa katika mechi ngumu kama ile unawapa kongole wachezaji na kuwaambia kuwa wamefanya vyema.

Kwa upande wake kocha wa Chelsea Guus Hiddink, alisema ilikuwa wazi kuwa Costa alitegwa kumzuia asifunge bao.