Crystal Palace yamsajili Adebayor

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Emmanuel Adebayor

Klabu ya soka ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu y England imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor.

Adebayor amesajiliwa na timu hiyo akiwa mchezaji huru kwa mkataba utamuweka chini ya meneja Alan Pardew mpaka mwisho wa msimu huu wa ligi.

Mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 31 aliachwa na timu yake ya Tottenham mwezi Septemba mwaka jana , na amefunga jumla ya magoli 94 katika Ligi ya England akiwa amezichezea timu za Tottenham,Arsenal na Manchester City.

Mara ya mwisho kwa mchezaji huyu kucheza mchezo wa ligi ilikua ni mwezi mei mwaka jana kwenye mchezo kati ya timu yake ya Tottenham na Man City .

Adebayor alijiunga na Arsenal, akitokea klabu ya Monaco, ya Ufaransa.kisha akajiunga na Man City kabla ya kupelekwa kwa mkopo kwa miamba wa soka wa Hispania Real Madrid na mwaka 2012 akajiunga na Tottenham.