Pat Fry ajiunga na timu Manor

Image caption Pat Fry wa Formula one

Timu ya magari yaendayo kasi ya Fomula1 ya Manor imeongeza bechi lake la ufundi baada ya kumchukua Pat Fry.

Fry aliyekua anakwenda kuwa mshauri wa ufundi kwenye masuala ya injini na kuwa mtu wa pili kutoka timu ya Ferrari kujiunga na Manor wa kwanza alikua ni mkuu wa kitengo cha ubunifu Nikolas Tombazis.

Ferrari walimfuta kazi Fry mwishoni mwa mwaka 201, na usajili wa mtaalamu huyu8 ni kuongeza nguvu kwa timu hiyo ili ikweze kufanya vizur msimu huu.

Fry mwenye miaka 51 ataunga na Dave Ryan ambae walikua wote timu ya McLaren na tayari timu hiyo ya Manor imeingia mkataba wa kutumia injini za Mercedes.