Azam,Simba,Yanga zasonga 16 bora

Image caption Timu ya Azam Fc

Timu za Azam FC, Simba SC, Yanga zimeungana na timu nyingine saba kufuzu kwa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho .

Michezo ya mzunguko wa nne ikitarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi Februari,

Jumla ya michezo 10 mpaka sasa imeshachezwa na timu kumi kujikatia tiketi ya kucheza mzunguko wa nne, ambao utazikutanisha jumla ya timu 16 mwezi ujao kusaka timu nane zitakazosonga mbele hatua ya nane bora.

Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora mpaka sasa ni Azam FC, JKT Mlale, Mwadui FC, Ndanda FC, Panone FC, Rhino Rangers, Simba SC, Tanzania Prisons, Toto Africans na Young Africans.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu, ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF