Leicester yasaka saini ya nahodha wa Nigeria

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ahmed Musa

Viongozi wa ligi ya Uingereza Leicester bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa licha ya ombi lao la hapo awali kukataliwa na kilabu ya CSKA Moscow kulingana na BBC michezo.

Kilabu hiyo ya Urusi imekataa ombi la dola milioni 21.6 huku wakitaka kiasi cha dola milioni 27 kumuachilia mshambuliaji huyo.

Mchezaji huyo yuko tayari kujiunga na kilabu hiyo.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Nigeria ana thamani ya dola milioni 32 katika kandarasi yake ambayo inakamilika mwaka 2019.

Leicester inatarajiwa kurudi kwa CSKA na kiasi cha juu ili kumchukua mchezaji huyo kabla ya kipindi cha dirisha la uhamisho kukamilika tarehe 1 mwezi Februari.