CHAN: Nigeria imetupwa nje na Guinea

Haki miliki ya picha CAF
Image caption CHAN: Nigeria imetupwa nje na Guinea

Timu ya Super Eagles ya Nigeria imeondolewa kutoka kwenye mashindano ya kuwania kombe la taifa bingwa la Afrika miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi za nyumbani.

Vigogo hao wa soka ya Afrika hawakuwa na jibu ya bao la Ibrahima Sankhon lililoiweka Guinea mbele kunako dakika 45 ya kipindi cha kwanza.

Super Eagles ilianza mechi hiyo ikihitaji ushindi ama hata sare ya aina yeyote kusonga mbele lakini Guinea ilikuwa na mipango tofauti.

Na baada ya nipe nikupe na mechi iliyokuwa na kasi , Guinea walifunga bao na kisha wakarejea nyuma kulinda lango lao.

Guinea hata hivyo walimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya wapinzani wao wakuu Tunisia.

Tunisia walithibitisha wao ni moto wa kuotewa mbali baada ya kuiadhibu vikali Niger mabao 5-0 .

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Nyamirambo

Haki miliki ya picha CAF
Image caption Tunisia walithibitisha wao ni moto wa kuotewa mbali baada ya kuiadhibu vikali Niger mabao 5-0

Kufuatia ushindi huo Tunisia inaongoza kundi hilo la Cha ikifwatwa kwa karibu na Guinea.

Washindi hao wawili sasa watasubiri hadi kesho kujua nani watakayechuana nao kati ya Uganda na Zimbabwe

Awali Cameroon ilijikatia tikiti ya kusonga mbele kwa kuinyuka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo 3-1.

Vilevile Ethiopia iliambulia kichapo cha 1-2 dhidi ya Angola.

Mechi inayotazamiwa na wengi ni ile kati ya DRC dhidi ya Amavubi ya Rwanda.

Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa taifa wa Amaghoro.#CHAN2016