Bodi ya tenisi kuchunguza tuhuma

Maafisa wa mchezo wa tenisi watachukua maamuzi ya uchunguzi binafsi kuyapeleka kwenye kamati ya kupambana na rushwa baada ya kuwa na tuhuma za kupangwa matokeo katika michezo ya tenesi.

Tangazo lililotolewa katika michuano ya wazi ya Australia, kufuatia uchunguzi wa BBC na BuzzFeed ambao unaonyesha kumekua na kupanga matokeo kinyume na sheria katika muongo uliopita.

Makabrasha yanaonyesha kwa miaka 10, iliyopita wachezaji 16, ambao waliokuwa katika kundi la wachezaji 50 bora wamekua wakijirudia rudia,hivyo kamati ya uadilifu ya tenisi (Tiu) imekua na hofu ya kupangwa kwa mechi pia.

Haki miliki ya picha

Wachezaji wote ikiwemo washindi wa mataji ya Grand Slam wameruhusiwa kuendelea na michuano hiyo.

Lengo la mapitio ni kulinda uadilifu wa mchezo lilisema tamkao la pamoja la ATP, WTA,pamoja na Shirikisho la Kimataifa la tenisi (ITF) na wakuu wa wote wanne Grand Slams.

Mwenyekiti wa Wimbledon Phillip Brook amesema "Ni maamuzi muhimu na viongozi wote wa mchezo wa tenesi tuko nyuma yake, tuko tayari kufanya chochote kuondoa rushwa katika mchezo wetu