Newcastle yamsajili Townsend

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Andros Townsend

Klabu ya soka Newcastle United imesajili winga wa kimataifa wa Uingereza Andros Townsend kwa gharama ya pauni milioni 12 akitokea Tottenham Hotspur.

Winga huyu mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kukitumikia kikosi cha Newcastle chini ya meneja Steve Mclaren.

Townsend amecheza michezo mitatu ya msimu huu akitokea benchi huku akiondolewa katika kikosi kilichokua kinashiriki michuano ya Europa ligi baada ya kugombana na kocha wa viungo Nathan Gardiner.

Meneja wa Newcastle United Steve McClaren, Amesema"kumleta winga huyu katika timu hiyo ni usajili mzuri na mkubwa, Andros ni aina ya mawinga wanaocheza staili ya kizamani anaweza cheza kulia na kushoto ."

Townsend alijiunga na kituo cha michezo cha Spurs akiwa na miaka nane na alianza kukitumiki kikosi cha kwanza katika msimu wa 2013-14.