Tenisi:Jopo la kumaliza ufisadi labuniwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jopo la kumaliza ufisadi katika mchezo huu kuundwa

Mamlaka za mchezo wa Tennis duniani zimetangaza kuunda jopo uhuru kuangazia jinsi ya kumaliza ufisadi katika mchezo huo.

Tangazo hili limetolewa katika michuano inayoendelea ya Australian Open.

Hii inafuatia uchunguzi wa BBC na mtandao wa BUZZFEED kwamba wachezaji 16 kwenye orodha ya 50 bora wamekua wakichunguzwa na kamati ya maadili ya mchezo huo kwa kushukiwa kupanga matokeo.

Maafisa wa mchezo huo wamezitaka serikali kuweka sheria inayoharamisha kupanga matokeo.

Rais wa shirikisho la mchezo wa Tennis, {ATP},Chris Kermode, amewaambia waandishi wa habari uchunguzi huu ni hatua ya kurejesha imani kwa mchezo wa Tennis.