Man United kuivaa Derby Kombe la FA

Klabu ya soka ya Manchester United, watajitupa ugenini katika dimba la iPro kuwakabili Derby County, katika hatua ya nne ya kombe la FA.

Man United watakua na presha kubwa ya mchezo huo baada ya timu hiyo kutokua na mwenendo mzuri huku kocha wake Luis Van Gaal akishutumia kwa timu hiyo kuboronga.

Kiungo Michael Carrick huenda akareje katika mchezo huo baada ya kukosa michezo minne kwa sababu ya majeraha,huku beki Matteo Darmian akiukosa mchezo huo sambamba na Bastian Schweinsteiger na Phil Jones ambao pi hawajajumuishwa kwenye kikosi hicho.

Derby wao wapo Nafasi ya 6 kwenye Msimamo wa Ligi daraja la kwanza (Championship) nao wendo wao si mzuri wakiwa hawajashinda michezo mitano iliyopita ya ligi.

Huu utakua ni mchezo wa 104 kwa timu hizi mbili kukutana na mara ya mwisho Derby Couty, wanaifunga Man U, ilikua ni kwenye kombe la ligi 2008.