Van Gaal: Sijakusudia kujiuzulu

Gaal Haki miliki ya picha PA
Image caption Van Gaal amekabiliwa na matatizo kutokana na Man Utd kuandikisha msururu wa matokeo mabaya

Meneja wa Manchester Louis van Gaal amesema hana mipango ya kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wake na kushutumu sana habari ambazo zimekuwa zikienea kwenye vyombo vya habari.

United wameshinda mechi tatu pekee kati ya 13 walizocheza karibuni ligini na karika shindano la kombe.

Van Gaal na wachezaji wenzake walizomewa na mashabiki baada ya kushindwa 1-0 na Southampton Jumamosi mechi ya Ligi ya Premia jambo lililofufua tena uvumi kuhusu hatima yake.

"Ni mara ya tatu kwangu kufutwa (kwenye vyombo vya habari) na bado niko hapa,” amesema Van Gaal.

United wamo nambari tano ligini, alama 10 nyuma ya viongozi Leicester City zikiwa zimesalia mechi 15.

Manchester United watakuwa ugenini dhidi ya Derby County katika raundi ya nne ya Kombe la FA Ijumaa.