Florent Malouda ajiunga na kilabu ya Misri

Image caption Florent Malouda

Kilabu ya Misri Wadi Degla imemsajili aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na Chelsea Florent Malouda.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amejiunga kutoka kilabu ya Delhi Dynamos nchini India ambapo amekuwa akisakata soka yake tangu mwaka 2015 mwezi Agosti.

Ameandikisha mkataba hadi mwisho wa msimu na anajiunga na mchezaji mwenzake wa Ufaransa Patrice Carteron ambaye alikuwa mkufunzi wa kilabu hiyo mapema mwezi Januari.

Malouda ambaye ameichezea Chelsea kutoka mwaka 2007 hadi 2013,aliichezea Ufaransa mara 80 na kufunga mbao tisa ya kimataifa.