Andy Murray afika fainali Australian Open

Djokovic Haki miliki ya picha AFP
Image caption Murray atakutana na Novak Djokovic kwenye fainali

Mwanatenisi nambari mbili duniani Andy Murray amefika fainali ya mashindano ya Australian Open mara ya tano baada ya kumshinda raia wa Canada Milos Raonic.

Mwingereza Murray alishindwa kwenye seti ya kwanza na ya tatu lakini mwishowe akaondoka na ushindi.

Murray, 28, alishinda 4-6 7-5 6-7 (4-7) 6-4 6-2 kwenye shindano hilo lililodumu saa nne mjini Melbourne.

Murray sasa atakutana na bingwa wa tenisi duniani Novak Djokovic kwenye fainali Jumapili.

Ushindi wa Murray dhidi ya Raonic, 25, unamfanya yeye na nduguye Jamie kuwa ndugu wa kwanza katika enzi ya mashindano ya Open kufika fainali za wanaume kwa mchezaji mmoja na wanaume wachezaji wawili katika shiindano la Grand Slam.

Jamie Murray na Bruno Soares watacheza dhidi ya Daniel Nestor na Radek Stepanek katika fainali ya wachezaji wawili wawili Jumamosi.