Mbia ajiunga na Gervinho nchini Uchina

Stephane Mbia Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mbia ameichezea Cameroon mara 67

Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina.

Mbia amekuwa akichezea Trabzonspor ya Uturuki.

Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 29 sasa atajiunga na nyota wa Ivory Coast Gervinho katika klabu hiyo ya Uchina.

Gervinho alijiunga na Hebei China Fortune akitokea AS Roma Jumatano.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Stephane Mbia wakati wa Kombe la Dunia nchini Brazil 2014

"Twamsubiri sana beki kamili Mbia afike hapa na kuonyesha ustadi wake,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter.

Mbia aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Najivunia kujiunga na Hebei China Fortune, niko tayari. Twende kazi."