Chelsea yailiza MK Dons

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Oscar Santos aliifungia Chelsea mabao matatu

Timu ya soka ya Chelsea hapo jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 5-1 walipocheza na MK Dons katika Mechi ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP iliyochezwa huko mk Denbigh Stadium, Mjini Milton Keynes.

Ushindi huo wa Chelsea umepatikana kupitia magoli matatu ya mchezaji wake Oscar, pamoja na Bao la Eden Hazard la Penati, ikiwa ni Bao lake la kwanza katika Mechi 28, na lile la Bertrand Traore.

Everton nao walitinga Raundi ya 5 kwa kushinda Ugenini kwa kuichapa Carlisle 3-0 kwa Bao za Arouna Kone, Aaaron Lennon na Ross Barkley.

Sasa Chelsea na Everton zinaungana na Timu nyingine 16 zikiwemo zile zitakazocheza mechi za marudiano kwenye Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 5.

Ambapo ratiba mpya inaonyesha kuwa michuano hiyo itaendelea tena Februari 19 hadi 22, Chelsea itakwaana na Manchester City, Reading dhidi ya West Brom au Peterborough,Watford watapepetana na Leeds United, Shrewsbury Town dhidi ya Manchester United, Blackburn watawavaa Liverpool au West Ham,Tottenham na Crystal Palace , Arsenal watakuwa wenyeji wa Hull na Bournemouth dhidi ya Everton