Maafisa wa riadha kukata rufaa CAS

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maafisa wanaoshutumiwa kwa rushwa ni Massata Diack,Valentin Balakh-nichev na Alexei Melnikov

Maafisa watatu wa mchezo wa riadha waliopigwa marufuku kujihusisha na maswala ya michezo kwa madai ya kujihusisha na rushwa wamedai kuwa watakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Maofisa hao ni Papa Massata Diack, ambaye ni mtoto wa mwana wa riadha wa zamani Lamine Diack, Mrusi Valentin Balakh-nichev na Alexei Melnikov.

Maofisa hao walishtakiwa mnamo mwezi Desemba mwaka jana kwa kosa la ukiukaji wa sheria za kupambana na madawa ya kulevya yanayomkabili Liliya Shobukhova.

Diack na Balakhnichev, rais wa zamani wa shirikisho la riadha la Urusi na mweka hazina,wa shirikisho la riadha IAAF walipigwa faini ya paundi 17,000 wakati kocha wa Urusi Melnikov alipigwa faini ya paundi 10,000.