Thamani ya uhamisho imezidi pauni bilioni 1

Haki miliki ya picha EPL
Image caption Thamani ya uhamisho imezidi pauni bilioni 1

Kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa ligi kuu ya Uingereza ,thamani ya uuzaji na malipo ya wachezaji,umegonga pauni bilioni moja.

Pauni milioni £965m zilitumika msimu uliopita wa mwaka wa 2014-15,

Huku zikisalia saa chache kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji katika ligi kuu ya Premia ya Uingereza rekodi mpya imeshawekwa.

Vilabu 20 vya ligi ya premia vimetumia takriban pauni milioni £130 kuanzia Januari mosi-31.

 • Klabu ya Newcastle imetoa pauni milioni £29m.

  Ligi ya pauni bilioni moja

  £1 bilioni

  Gharama ya kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho la ligi ya Premia mwaka 2015/16

  • £130 milioni pesa zilizotumika katika dirisha dogo la Januari

  • £29m Kiwango kilichotumiwa na klabu ya Newcastle United

Newcastle imewanunua Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet.

Vilevile timu hiyo imeweka dau ya paundi milioni £21m kwa ajili ya kununua huduma za mshambulizi wa West Brom Saido Berahino.

Afsa mmoja wa kampuni ya urasimu ya Sports Business Group at Deloitte, Dan Jones, amesema kuwa '' kwa mara nyengine tumeshuhudia vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya uingereza vikiwekeza kiasi kikubwa mno cha fedha ilikusajili ufundi na huduma za wachezaji.''

"Hii ndio mara ya kwanza kwa thamani ya uhamisho kuzidi pauni bilioni moja''