Chelsea,Watford zashindwa kufungana

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Chelsea na Watford zatoshana nguvu

Klabu ya soka ya Chelsea jumatano imetoshana nguvu na Watford kufuatia sare ya kutofungana, huku Everton wao wakifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa bao 3-0 dhidi ya Newcastle ikiwa ni mwencelezo wa Ligi kuu ya England.

Na Timu ya soka ya Barcelona usiku wa jana ilishusha gharika ya magoli baada ya kuichapa Valencia bao 7-0, katika mwendelezo wa michuano ya kombe la mfalme.

Magoli ya Barcelona yamefungwa na wachezaji Luis Suárez bao (4) na Lionel Messi bao (3).