Roger Federer kuwa nje baada ya majeraha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Roger Federer

Mchezaji bora namba tatu wa Dunia katika mchezo wa Tenisi Roger Federer atakuwa nje ya uwanja kwa muda mwezi baada ya kuumia goti.

Federer mwenye miaka 34 ambaye ni mshindi mara 17 wa Grand Slam aliumia wakati wa mashindano ya wazi ya Australian huku akiondoshwa katika hatua ya nusu fainali na Novak Djokovic wiki iliyopita.