Ubelgiji vinara viwango ubora vya Fifa

Haki miliki ya picha epa
Image caption Ubelgiji inaongoza viwango vya ubora vya Fifa

Ubelgiji imeendelea kukaa katika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora vya FIFA kwa muhjibu wa viwango viliyotolewa Alhamisi.

Katika kumi Bora imebaki vile vile bila mabadiliko huku Mabingwa wa Dunia, Germany, wakiwa Nafasi ya 4.

Ivory Coast imeporomoka hadi Nafasi ya 9 kwa bara la afrika na sasa ipo Nafasi ya 28 Duniani ikifuatiwa na Cape Verde ambayo ipo Nafasi ya 33 baada ya kupanda Nafasi huku Algeria ikiwa Nafasi ya 36 baada ya kushuka Nafasi 8.

Timu nyingine katika ishirini bora ni Ubeligiji, Argentina, Uhispania, Ujerumani na Chile.

20 bora katika viwango vya Fifa.

1 Ubelgiji

2 Argentina

3 Uhispania

4 Ujerumani

5 Chile

6 Brazil

7 Portugal

8 Colombia

9 England

10 Austria

11 Uruguay

12 Switzerland

13 Ecuador

14 Uholanzi

15 Italy

16 Romania

17 Wales

18 Croatia

19 Hungary

20 Uturuki