Ubaguzi waitia mashakani Kilabu ya Lazio

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashabiki soka

Kilabu ya Lazio imepigwa faini ya £38,250, baada ya mechi yao dhidi ya Napoli, iliyochezwa siku ya jumatano usiku, kusimamishwa kwa muda, baada ya mashabiki wa klabu hiyo kuanza kutumia lugha ya ubaguzi.

Kilabu hiyo ya Roma, sasa italazimika kufunga maeneo matatu ya uwanja wao wa nyumbani wa Stadio Olimpico, wakati wa mechi zao mbili za nyumbani.

Mechi hiyo ilisimamishwa kwa dakika tatu katika kipindi cha pili baada ya mashabiki kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya mlinda lango wa Napoli, Kalidou Koulibaly.

Napoli, inayoongoza ligi kuu kwa sasa ilishinda kwa magoli mawili kwa bila.

Mchezaji huyo kutoka Senegal, alimpongeza refa wa mechi hiyo kwa kusimamisha mechi hiyo.

Baada ya mechi hiyo meneja wa Lazio, alisema angelikuwa refa pia angelisimamisha mechi hiyo.

Amesema ni mashabiki wachache tu ndio waliohusika, ila hadhani yalikuwa ya ubaguzi. Amesema pia kilabu hiyo inawachezaji walio na asili ya Kiafrika.

Kilabu hiyo imeadhibiwa mara kadhaa siku zilizopita kutokana na makosa kama hayo.

Msemaji wa ligi kuu nchini humo amesema mbali na faini hiyo klabu hiyo ya Roma, italazimika kufunga maeneo hayo mawili kama njia moja ya kudhibiti mashabiki wao.