Rosicky nje kwa jeraha la miezi mitatu

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Tomas Rosicky

Kiungo wa kati wa kilabu ya Arsenal Tomas Rosicky hatochezea timu yake kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na jeraha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye kandarasi yake inakamilika katika msimu wa joto,alipata jeraha jingine la paja wakati wa mechi dhidi ya Burnley siku ya jumamosi baada ya kipindi cha miezi saba akiuguza jereha.

Mchezaji huyo wa taifa la Czech alijiunga na Arsenal mnamo mwezi Mei mwaka 2006.

Alipoulizwa iwapo Rosicky ameichezea Arsenal mechi yake ya mwisho,Wenger alijibu:Natumai hapana ,lakini jeraha hilo ni baya sana.Rosicky ambaye aliichezea Arsenal mara 246 alisaini mkataba wa mwaka mmoja msimu uliopita.

wenger

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Wakati huohuo,Wenger amethibitisha kwamba mshambuliaji Danny Welbeck atarudi kuwachezea wachezaji wa Arsenal wasiozidi umri wa miaka 21 siku ya ijumaa.

Mchezaji huyo wa Uingereza,mwenye umri wa miaka 25,ameuguza jereha tangu mwezi Aprili 2015 baada ya kupata jeraha hilo katika mechi iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Chelsea.