Mke wa Andy Murray ajifungua msichana

Kim Haki miliki ya picha
Image caption Kim Sears alijaliwa mtoto wa kike Jumapili

Mke wa mchezaji tenisi mashuhuri Andy Murray, Kim Sears, amejifungua mtoto wa kike, BBC imebaini.

Mtoto wa kwanza wa wanandoa hao inaaminika kuwa alizaliwa Jumapili

Walioana katika mji anakozaliwa Murray wa Dunblane mwezi Aprili mwaka uliopita.

Murray, ambaye ni nambari mbili katika mchezo wa tenisi, alizungumzia kuhusu matarajio yake baada ya kuwa baba katika mashindano ya mwezi uliopita ya Australian Open, alisema kuwa familia yake itakuwa "kipaumbele".

Alisema bayana kwamba angelikatiza mchezo wake wa mwaka na kurejea nyumbani kama mwanaye angelizaliwa mapema kuliko ilivyotarajiwa .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Murray na Kim walifunga ndoa Aprili mwaka jana

Alisema: "Mwanangu ni muhimu zaidi kwangu, na mke wangu ni muhimu zaidi kwangu, kuliko mechi ya Tennis .

"Ni mabadiliko makubwa kwangu na kwa mke wangu, lakini kwa sasa ndio kipaumbele changu, na tutaona baada ya hilo.

"Sijui hilo litabadili vipi mambo. Bado napenda tenisi."

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Murray alishindwa na Djokovic fainali Australian Open

Murray aliweza kufika fainali katika Australian Open na huku akitokwa machozi alimweleza mkewe: “Naabiri ndege inayofuata kuelekea nyumbani.

Hii ni baada yake kushindwa kwenye fainali na Novak Djokovic.