Kamusoko mchezaji bora mwezi December

kiungo wa klabu ya Yanga Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania kwa mwezi disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa yanga Amissi Tambwe

Kamusoko ameisaidia timu yake katika michezo iliyochezwa mwezi disemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa disemba.

kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi disemba, atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi.