Morocco yamtimua kocha Zaki

Haki miliki ya picha .
Image caption Badou Zaki

Chama cha soka nchini Morocco Royal Moroccan Football Federation (FRMF) kimemfuta kazi kocha wake Badou Zaki.

Taarifa ya chama cha soka imesema "Baada ya miezi ishirini ya kukosekana kwa utulivu na matokeo mabaya tumekubaliana kufikia mwisho wa mkataba wake.

Chama cha soka kimesema kitangaza kocha mpya wa kikosi cha taifa siku chache zijazo,kocha wa zamani wa Ivory Coast Herve Renard, anatajwa kama kocha atayechukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho.

Zaki kipa wa zamani wa timu ya taifa mwenye umri wa miaka 56 alichukua mamlaka ya kuwa kocha wa timu hiyo kwa mara ya pili mwaka 2014. Kwa mara ya kwanza kocha huyu alikinoa kikosi hicho mwaka 2002.