Mido apigwa kalamu Zamalek

Image caption Aliyekuwa kocha wa Zamalek Mido

Aliyekuwa mshambuliaji wa kilabu ya Tottenham pamoja na Middlesborough Mido amefutwa kazi kama mkufunzi wa Zamalek kwa mara ya pili baada ya siku 37 akiongoza mabingwa hao wa Misri.

Mido mwenye umri wa miaka 32 ambaye aliifunza kilabu hiyo kwa miezi 6 mwaka 2014 aliajiriwa tena tarehe 4 mwezi Januari.

Alishinda mechi zake nne za kwanza,lakini sare moja na kushindwa mara moja na baadaye kufuatiwa na kushindwa 2-0 na wapinzani Al Ahly siku ya jumanne.

Hatua hiyo imeiwacha Al Ahly ikiwa pointi saba juu ya Zamalek katika kilele cha jedwali la ligi ya taifa hilo.

Mohamed Salah sasa amechukua ukufunzi wa kilabu hiyo kama kaimu kocha huku kilabu hiyo ikitafuta kocha mpya ugenini.

Mkurungezi wa soka Hazem Emam,ambaye aliajiriwa wakati huohuo na Mido pia amepigwa kalamu.