Fifa:Jerome Valcke apigwa marufuku

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jerome Valcke na aliyekuwa rais wa Fifa Sepp Blatter

Aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amepigwa marufuku kushiriki katika soka yoyote kwa kipindi cha miaka 12.

Uamuzi huo umeafikiwa na kamati ya maadili ya shirikisho hilo kufuatia madai ya uovu yanayohusishwa na uuzaji wa tiketi za michuano ya kombe la dunia.

Wakati wa uchunguzi ,visa kadhaa vya uovu vilijitokeza ,ikiwemo matumizi ya nauli,sera na taratibu.

Valcke pia amepigwa faini ya faranga 100,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 70,800.