MOJA KWA MOJA:Sunderland dhidi ya Manchester United

Katika Mechi ya jumamosi Kilabu ya Sunderland ambayo iko chini ya jedwali la ligi linakabiliana na kilabu ya Manchester United katika uwanja wa Stadium of Light.

19.30pm:Matokeo ya ligi ya Uingereza kufikia dakika ya 74

Bournemouth 1 - 3 Stoke

Crystal Palace 1 - 1 Watford

Everton 0 - 1 West Brom

Norwich 2 - 0 West Ham

Swansea 0 - 0 Southampton

18.54pm:Matokeo ya ligi kuu ya Uingereza kufikia kipindi cha mapumziko

Bournemouth 0 - 1 Stoke

Crystal Palace 1 - 1 Watford

Everton 0 - 1 West Brom

Norwich 0 - 0 West Ham

Swansea 0 - 0 Southampton

18.47pm:Gooooooooal Adebayor aisawazishia Crystal palace kunako dakika 45 ya kipindi cha kwanza

Crystal palace 1-1Watford

18.38pm:Matokeo ya ligi ya Uingereza kufikia sasa

Sunderland 2 - 1 Man Utd FT

Bournemouth 0 - 1 Stoke

Crystal Palace 0 - 1 Watford

Everton 0 - 1 West Brom

Norwich 0 - 0 West Ham

Swansea 0 - 0 Southampton

18.17pm:Crystal Palace 0- 1 Watford
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha wa United Van Gaal

17.39pm:Na mpira unakwisha ikiwa Sunderland wamefanikiwa kuichapa Manchester United.

17.38pm: la la la hatari hapa Sunderland yakosa bao la pili

17.37pm:Mkufunzi Van Gaal aangalia kopo la saa yake na wasiwasi

Sunderland 2-1 manchester United

17.35pm:Dakika nne za ziada zaongezwa.

Sunderland 2-1 manchester United

17.31pm:Kipa wa Sunderland aokoa shambulio kutoka kwa Anthony Martial

17.28pm:Makocha wa United wakiongozwa na Van Gaal na Ryan Giggs wakosa furaha

Image caption Sunderland wapata bao la pili

17.26pm:Gooooooooooal Sunderland yajipatia bao la pili

Image caption bao la Sunderland

82'' Sunderland 2-1 Manchester United

16.25pm:Sunderland yapata kona

16.23pm:Manchester United wakosa bao pale baada ya Memphis Depay kuupiga mpira kwa kipa.

17.21pm:Kona nyengine kuelekezwa katika lango la Sunderland.Manchester United inafanya mashambulizi

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wayne Rooney

17.91pm:Kona kuelekezwa kwa lango la Sunderland.

17.08pm:Mpira wa adhabu kuelekezwa lango la manchester United baada ya mchezaji wao kucheza visivyo

17.06pm:Kipa De Gea aokoa bao hapa kutoka kwa mshambulizi wa Sunderland baada ya kubaki na kipa.

17.03pm:Mechezaji mwengine wa manchester UnitedCarrick anapewa kadi ya njano baada ya kucheza visivyo.

Image caption Defoe atoka

17.02pm:Juan Mata anapewa kadi ya njano baada ya kucheza visivyo

17.01pm:Manchester sasa wanajaribu kupenya ngome ya Sunderland.

17.00pm:Mechi imeanza kwa kasi na kila timu inafanya mashambulizi hapa.

16.54pm:Sunderland inapata mpira wa adhabu. Kona

16.45pm:Kipindi cha pili cha mechi kinaanza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Anthony Martial

16.24pm:Gooooooal Manchester United wasawazisha kupiia bao lililofungwa na Anthony Martial

16.16pm:Mataaaaaaa kipa manone achukua mpira bila tatizo.

16.14pm:Manchester United yavamia lengo la Sunderland.

Image caption Nahodha wa kilabu ya Manchester United Wayne Rooney

16.08pm:Shambulizi la Sunderland lampiga mkono beki wa manchester United lakini refa asema hajaunawa mpira licha ya wachezaji wa Sunderland kulalama

16.04pm:Wachezaji wa United wajaribu kushambulia lango la Sunderland lakini mabeki wa timu hiyo wakataa

16.03pm:Mpira wa kurushwa kuelekea lango la manchester United.

16.01pm:Vijana wa Sunderland waonekana kurudi nyuma ili kulinda lango lao,huku washambuliaji wa Mancheester United wakilazimika kufanya kazi ya ziada

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jermaine Defoe

15.57pm:La.la.la Defoe akosa bao la wazi hapa katika lango la manchester United.

15.53pm:Manchester United inafanya mashambulizi katika lango la Sunderland lakini bahati haijasimama.

15.51pm:Manchester United sasa inaanza kutafuta bao kwa udi na uvumba ili kuweza kusawazisha.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkufunzi Van Gaal baada ya kufungwa kwa bao

15.48pm:Gooooooooal.Sunderland inapata bao lake la kwanza baada ya dakika tatu za mchezo,baada ya mpira wa adhabu kupigwa.

15.45pm:Mechi inaanza.Sunderland 0 0 Manchester United

Image caption wachezaji wa Sunderland

Sunderland

Image caption Wachezaji wa manchester United

Manchester United