TFF yaipongeza African Lyon

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeipongeza timu ya African Lyon FC ya jijini Dar es salaam kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu msimu ujao, baada ya kuwa vinara wa Kundi A katika ligi hiyo iliyomalizika jana.

African Lyon imeungana na timu ya Ruvu Shooting FC ya Mlandizi mkoa wa Pwani iliyokua timu ya kwanza kupanda ligi kuu wiki iliyopita kutoka kundi B.

TFF inaitakia kila la kheri Africa Lyon FC katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu , kwa kujiandaa vizuri na mikiki mikiki ya VPL ambayo ina jumla ya timu 16 na kila klabu kucheza jumla ya michezo 30 kwa msimu nyumbani na ugenini.