Cameroon yaishinda Misri voliboli

Haki miliki ya picha Guy Suffo CAVB

Katika Mechi ya Fainali ya mashindano ya voliboli ya wanawake afrika yaliyomalizika mjini Yaounde hapo jana, Cameroon imeishinda Misri kwa seti 3-2.

Kwa ushindi huo Cameroon italiwakilisha bara Afrika katika michezo ya Olimpiki mwezi Agosti mjini Rio Brazil.

Katika mechi ya kuwania mshindi wa tatu Kenya imewashinda Algeria seti 3-0 na kuzoa nishani ya shaba.

Nafasi ya tano imetwaliwa na Botswana, ikifuatiwa na Botswana na Uganda ikawa ya mwisho.