Manny Pacquiao aomba radhi

Haki miliki ya picha Getty

Mwanamasumbwi Manny Pacquiao amelazimika kuomba radhi kutokana na upinzani mkubwa alioupata kutoka kwa wale wanaounga mkono uhusiano ya jinsia moja.

Sakata hili limeanza pale ambapo Pacquaio ambaye pia ni mbunge huko kwao ufilipino aliposema kupitia televisheni kuwa matendo ya jinsia moja ni mabaya kuliko ya wanyama.

Mwanandondi huyo alisema, kwa akili ya kawaida hata wanyama wanajua huyu dume huyu jike, mnyama dume hampandi mnyama dume na jike hampandi mnyama jike, kwa hivyo wanadamu tukiruhusu uhusiano wa jinsia moja basi tunafanya matendo mabaya kuliko hata hao wanyama.

Watu walipomzonga sana, akaweka mtandaoni , picha yake akiwa na mkewe, sasa wamemzonga zaidi kawaomba msamaha lakini akawaambia nimeusema ukweli kama ulivyo kwenye misahafu, Mungu awabariki na ninawaombea.