Nike yasitisha mkataba na Manny Pacquiao

Kampuni ya utengenezaji vifaa vya michezo ya Nike, imesitisha mkataba na uhusiano na mwanamasumbwi Manny Pacquiao baada ya bondia huyo wa uzito wa juu dunia baada ya kuwafananisha wapenzi wa jinsi moja kama wasio na thamani zaidi ya wanyama.

Bingwa huyo wa masumbwi ulimwenguni mwenye umri wa miaka 37, ambaye anagombea nafasi ya useneta katika bunge nchini mwake Phillipines, ingawa baadaye aliomba radhi baada ya kuzongwa na dunia kwa kauli yake hiyo.

Kampuni ya NIKE imetoa tamko lake kwa kusema kuwa kauli ya Manny Pacquiao kama yenye ufinyu wa mawazo.

Katika tamko hilo, Nike inapinga ubaguzi wa ina yoyote ile na kwamba kampuni hiyo imejiwekea historia ya kuwaunga mkono na kutetea misimamo yake dhidi ya haki ya jamii ya wapenzi wa jinsi moja .

Kampuni hiyo ianayojishughulisha na vifaa vya michezo ikaongeza kusema kwamba inavunja uhusiano na mkata na Manny Pacquiao.

Kauli hiyo ya Pacquiao aliitoa wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano kwenye runinga na awali alionekana kutojutia kauli yake hiyo lakini baadaye katika akaunti yake ya Instagram akaitetea kauli hiyo kwa kusema kwamba alikuwa akisema ukweli kwa muujibu wa kilichoandikwa kwenye Biblia takatifu.

Hata hivyo,baadaye bondia huyo akaandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba alikuwa haishambulii jamii hiyo ya wapenzi wa jinsi moja,wakati bado alipokuwa akielezea upinzani wake kwa ndoa za mashoga.

Katika pambano lake la mwisho mnamo mwezi mei mwaka wa jana ,pacquiao, alipigwa na Floyd Mayweather , Pacquiao, anatarajiwa kuingia ulingoni kumkabili Mmarekani Timothy Bradley Jr mjini Las Vegas mwezi April mwaka huu.