Ronaldo awajibu waandishi kwa vitendo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Christiano Ronaldo

Christian Ronaldo ni kama amewajibu kwa vitendo wanahabari wale ambao jumanne alikataa kuendelea kuongea nao pale alipoulizwa kuhusu ukame wa magoli ya ugenini. Goli lake la 33 la Musimu limeisaidia Real Madrid kusogelea robo fainali ya Champions Ligi. Kikosi kilichoko chini ya Zinedine Zidane kimeichapa Roma bao mbili kwa moja.

Kabla ya Mechi hiyo Mshambuliaji huyo alikuwa ameondoka kwa hasira katika katika chumba cha mahojiano baada ya kuulizwa juu ya rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za ugenini msimu huu.

Ronaldo mwenye miaka 31, mpaka hapo alikuwa amefunga magoli 32 msimu huu lakini hakuwa amefunga nje tangu mwezi Novemba. "Nani mwingine amefunga magoli mengi ugenini kuliko mimi tangu nimekuja Hispania?Ronaldo mfungaji namba moja wa Championzi Ligi aliuliza kwa kukereka" Taja mchezaji mmoja ambaye amefunga kuliko mimi. Hakuna jibu? Sawa. Asante" Akaondoka.